1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Serbia apinga uhuru wa Kosovo

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTXa

Rais wa Serbia, Boris Tadic, anayeshiriki katika mazungumzo ya mwisho kuhusu hatima ya jimbo la Kosovo mjini Vienna Austria, ameonya kwamba hataliruhusu jimbo hilo liwe huru kutoka kwa Serbia.

Maafisa wa vyeo vya juu wa jimbo la Kosovo na Serbia wanakutana na wapatanishi wa Umoja wa Ulaya, Urusi na Marekani kujadili mapendekezo kadha lakini matumaini ni machache kwamba watafaulu kupata suluhisho.

Walbania wa Kosovo wanasema watatangaza uhuru kutoka kwa Serbia baada ya tarehe 10 mwezi ujao.

Serikali ya Serbia mjini Belgrade, ikiungwa mkono na mshirika wake mkubwa Urusi, inataka jimbo la Kosovo liwe tu na uhuru wa kujitawala, lakini liendelee kubakia sehemu ya Serbia.