1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Serbia adai ushindi wa chama chake uchaguzi wa Bunge

18 Desemba 2023

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic amedai kuwa chama chake cha Serbian Progressive Party (SNS), kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge uliofanyika jana Jumapili.

https://p.dw.com/p/4aIDl

Rais Aleksandar Vucic wa Serbia amedai kuwa chama chake cha Serbian Progressive Party (SNS), kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge uliofanyika jana Jumapili, na hivyo kukiwezesha kusalia madarakani katika nchi hiyo ya Balkan. 

Vucic amesema baada ya karibu asilimia 76 ya kura kuhesabiwa, watakuwa na wingi wa viti bungeni kwa kuwa na viti 127 kati ya 250. 

Matokeo rasmi yamepangwa kutangazwa leo jioni lakini upinzani tayari wamesema kuwa udanganyifu umefanyika katika mchakato huo.

Soma pia: Serbia na Kosovo wakutana kwenye mazungumzo ya kuskaa suluhu

Machapisho kwenye mitandao ya kijamii yamechochea pia uvumi kwamba serikali iliruhusu wapiga kura ambao hawajajiorodhesha kutoka nchi jirani ya Bosnia kupiga kura kinyume cha sheria. 

Waziri Mkuu wa Serbia Ana Brnabic ametupilia mbali madai hayo na kusema yana lengo la kuzusha machafuko.