1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Bayern Munich akubali kwenda jela

16 Machi 2014

Rais wa Klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness akubali kwenda jela miaka mitanu unusu, kwa kukwepa kulipa kodi nchini Ujerumani, na klabu hiyo sasa inajitayarisha kuendelea na maisha bila ya kiongozi huyo.

https://p.dw.com/p/1BQQi
Prozess Uli Hoeneß Steuerhinterziehung 13.03.2014
Rais wa zamani wa klabu ya Bayern Munich Uli HoenessPicha: Reuters

Siku moja baada ya kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa mamilioni ya kodi , Uli Hieness rais wa klabu maarufu ya Bayern Munich jana Ijumaa alitangaza kuwa hatakata rufaa dhidi ya hukumu dhidi yake ya kwenda jela miaka mitano unusu na atajiuzulu kutoka nyadhifa zake kama rais wa Bayern, klabu maarufu na yenye mafanikio makubwa katika soka nchini Ujerumani na Ulaya kwa jumla.

Wakili wake hapo kabla alisema kuwa atakata rufaa kwa niaba ya mteja wake dhidi ya hukumu hiyo ambapo alikutikana na hatia ya kukwepa kulipa kiasi cha euro milioni 28.5 za kodi.

Prozess Uli Hoeneß Steuerhinterziehung 13.03.2014
Uli HoenessPicha: Reuters

Mafanikio

Bayern Munich ni kazi ya maisha yangu na inabaki daima kuwa hivyo, amesema Hoeness katika taarifa, akiongeza kuwa ana matumaini kuiepusha klabu hiyo na madhara yoyote mengine kwa kuamua kujiuzulu. Nitaendelea kuhusika na klabu hii muhimu na watu wake katika njia nyingine muda wote nitakapokuwa hai, amesema Honness.

Mahusiano yoyote mengine ambayo Hoeness atakuwa nayo na Bayern , uamuzi wake una maana kuwa vigogo hivyo vya soka la Ujerumani , mabingwa wa sasa wa champions League barani Ulaya , yatakuwa bila ya kiongozi huyu kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 44.

Hoenness ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 62, amepata mafanikio makubwa akiwa kama mchezaji na klabu hiyo ya mjini Munich , ambapo alijiunga na klabu hiyo mwaka 1970, akishinda vikombe vitatu vya ulaya. Lakini ni katika utendaji wake kama meneja mkuu ambapo aliibadilisha Bayern Munich kuwa moja kati ya vilabu vikubwa barani Ulaya.

Akikubali wadhifa mwaka 1979 akiwa na umri wa miaka 27 , muda wake wa kucheza kandanda ukiwa umemalizika mapema kutokana na kuwa majeruhi, Hoeness alitumia uwezo wake wa kibiashara na kampuni yake ya kutengeneza nyama za soseji barani Ulaya kuleta wafadhili na vitega uchumi katika muda wote wa uongozi wake wa miaka 31 katika klabu hiyo. Katika maelezo aliyoyatoa katika kituo cha televisheni cha taifa ARD mwenyekiti wa shirika linalopambana na rushwa duniani Transparency International nchini Ujerumani Caspar von Hauenschild amesema viatu vya Uli Hoenness ni ngumu kuvivaa wakati huu.

"Katika kila baraza la ushauri, mwenyekiti wa baraza hilo ndie mwenye mamlaka makuu, katika shirika lolote lile. Wakati inapotakiwa kuchukua maamuzi magumu sauti yake inakuwa nzito. Uzito wa sauti hii kwa Uli Hoeness kwa mtazamo wangu si rahisi kwa kweli kuipata tena."

Herbert Hainer Vorstandsvorsitzender Adidas
Rais mpya Herbert HainerPicha: AP

Hoennes alikuwa rais wa Bayern Munich mwaka 2010, na mafanikio yaliendelea, kwa timu hiyo kushinda mataji matatu kwa msimu mmoja mwaka jana 2013.

Mwenyekiti mpya ateuliwa

Kile anachokiacha Hoeness kwa klabu hiyo ni kwamba kuondoka kwa Hoennes itakuwa si rahisi lakini si kwanza haitawezekana kuiendeleza hali hiyo ya mafanikio. Bidhaa ambayo ni Bayern Munich itaendelea kuvutia soko duniani kote, wakati kikosi cha timu hiyo kina uwezo mkubwa hivi sasa katika Bundesliga ambapo fedha zinazopatikana kutoka katika kushiriki katika champions league hazitakatika.

Wakati huo huo Herbert Hainer ameteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa baraza la ushauri la Bayern Munich , klabu hiyo imetangaza siku ya Ijumaa.

Klabu hiyo ilifanya mkutano wake wa dharura kwa njia ya muunganisho wa simu saa chache baada ya Uli Hoenness kujiuzulu wadhifa wake kwa kuamua kutokata rufaa hukumu dhidi yake.

Tukirejea zaidi katika soka tuelekee sasa huko nchini Uingereza ambapo kesho Jumapili kutakuwa na mpambano wa kukata na shoka wakati Manchester United itakapokwaana na mahasimu wao wa Liverpool , ambapo mara hii Liverpool inaonekana kuwa ndio wenye uwezo mkubwa wa kuishinda Liverpool kinyume na miaka kadha iliyopita.

Ushindi mara nne mfululizo umekifanya kikosi hicho cha kocha Brendan Rodgers kuingia katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi, points saba nyuma ya Chelsea ikiwa na mchezo mmoja zaidi. Ikiwa Liverpool itafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Manchester kesho Jumapili itapunguza mwanya hadi points tano na kuzungumzia kupata taji hilo la Premier League kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990.

FC Everton Trainer David Moyes
Kocha wa Man U David MoyesPicha: Getty Images

Liverpool haijacheza katika ligi tangu ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Southampton Machi mosi, lakini Rodgers hana wasi wasi kwamba nguvu walioijenga inaweza kuzimwa.

El-Clasico

Na huko katika ligi ya Uhispania kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti ameitaka timu yake kuendelea kukata mbuga kama viongozi wa ligi wakati wakielekea huko Malaga kwa mchezo muhimu wa ligi jioni ya leo kabla ya kukumbana na Barcelona katika kile kinachojulikana kama el-clasico mwishoni mwa juma lijalo.

Madrid wako points tatu mbele ya Atletico Madrid na points nne mbele ya Barcelona na watakuwa na nia ya kupanua mwanya huo na kuendeleza ushindi katika michezo 29 bila kufungwa dhidi ya Malaga timu ambayo inahangaika kujiokoa kushuka daraja.

Carlo Ancelotti Trainer Paris Saint-Germain
Kocha wa Real Madrid Carlo AncelottiPicha: Franck Fife/AFP/Getty Images

Lakini Ancelotti ameielezea hali ya timu hiyo kama paa anayejaribu kuepuka makucha ya simba anayemfukuza.

Katibu mkuu wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Jerome Valcke anaamini kuwa kuna hali ya kukimbilia muda katika ukamilishaji katika muda muafaka wa kila kitu nchini Brazil kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia Juni 12 mwaka huu.

Akizungumza katika mahojiano katika tovuti ya FIFA jana Ijumaa, Valcke amesema kuwa sio tu FIFA lakini pia watayarishaji nchini Brazil , serikali ya Brazil na miji wenyeji wa mashindano hayo wanalazimika kufanya haraka.

Ukweli ni kwamba , ingekuwa vizuri iwapo viwanja vingekuwa tayari mwezi Desemba 2013 na sio Machi 2014, amesema Valcke.

Eneo ambalo halijasakafiwa lenye ukubwa wa mita za mraba 140,000 kuzunguka uwanja wa mjini Porto Alegre ni miongoni mwa suala kuu linaloumiza vichwa vya viongozi wa FIFA ikiwa imebakia miezi mitatu hadi kuanza fainali hizo za kombe la dunia nchini Brazil, amesema katibu mkuu huyo wa FIFA Jerome Valcke siku ya Alhamis.

Mbio za magari.

Kampuni ya Red Bull imeshinda mataji manne ya dunia ya mbio za magari za Formula one lakini wakati msimu mpya unaanza mjini Melbourne kesho Jumapili(16.03.2014), Mercedes haitatumia utaratibu wa timu wa kusaidia mmoja wa madereva wao dhidi ya mwingine.

Formel 1 Australien Melbourne Sebastian Vettel
Magari ya formula onePicha: Getty Images

Tumekuwa na majadiliano , na wote tunataka kuona timu yetu ikiwa mbele lakini tunataka kuona madereva wote wakipambana kila mmoja dhidi ya mwingine, mkuu wa spoti wa kundi la Mercedes Toto Wolff amesema wiki hii.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman