1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Trump yuko Brussels

Admin.WagnerD25 Mei 2017

Rais Donald Trump wa Marekani Alhamisi (25.05.2017) anakutana na wakuu wa asasi za Umoja wa Ulaya mjini Brussels kabla ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO hapo baadae.

https://p.dw.com/p/2dYvH
Belgien Donald Tusk und Donald Trump
Picha: Getty Images/AFP/E. Dunand

Katibu Mkuu  wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg akichambuwa agenda ya mkutano wa leo wa viongozi wa NATO alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Barussels Ubelgiji amesema "Leo tutaamuwa kutanua msaada wetu kwa muugano huo kwa kuongeza muda wa safari za ndege za Iraq,kushirikiana zaidi taarifa za kijasusi na kujaza ndege mafuta hewani.Nchi zote wanachama 28 za muungano huo wa kimataifa leo zitakubaliana juu uwanachama wa NATO kwa muungano wao huo.Hatua hii itatowa ujumbe madhubuti wa kujitolea kwa NATO kupambana dhidi ya ugaidi."

Wanadiplomasia wanasema kujiunga kwa NATO katika mapambano yanayoongozwa na Marekani dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislam ni dai mhimu la Rais Donald Trump wa Marekani kwamba jumuiya hiyo inapaswa kuchukuwa hatua zaidi kupiga vita ugaidi wa Kiislamu.

Trump akiwa katika mkondo wake wa nne wa ziara yake ya kigeni alilakiwa na Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk na waziri mkuu wa zamani wa Poland ambaye ni mwenyekiti wa mikutano ya viongozi 28 wa Umoja wa Ulaya.Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean Claude Juncker pia atajiunga na mazungumzo hao ya Trump na viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Trump abadili msimamo kuhusu NATO

NATO Stoltenberg PK vor dem Gipfel in Brüssel
Katibu Mkuu wa Jumuiya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg.Picha: Reuters/H. Hanschke

Trump ambaye alielezea mashaka yake wakati alipokuwa katika kampeni ya uchaguzi wa rais nchini Marekani juu ya thamani ya NATO na hata kufikia kutamka kwamba jumuiya hiyo imepitwa na wakati na kupongeza kura ya Uingereza kujitowa Umoja wa Ulaya atapokea wito wa viongozi wa Ulaya wa kumtaka aendelee kushikilia msimamo wa muda mrefu wa serikali ya Marekani kuunga mkono kungana kwa mataifa ya Ulaya halikadhalika biashara uru na juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Trump alikuwa akitafakari kujitowa katika jumuiya hiyo kwa sababu alikuwa akiamini nchi nyengine wanachama zilikuwa hazitimizi wajibu wao katika kuichangia jumuiya hiyo na hadi sasa amegoma kujitolea kwa kifungu nambari 5 cha jumuiya hiyo chenye kuzilazimisha nchi wanachama kuapa kuzilinda nchi nyengine.

Hivi karibuni rais huyo amebadili msimamo kidogo kwa kupongeza umuhimu wa jumuiya hiyo na waziri wake wa mambo ya nje Rex Tillerson amesema bila ya shaka Marekani inaunga mkono kufungu hicho nambari tano isipokuwa tu inataka nchi zote wanachama kutumia asilimia mbili ya pato lao la jumla kwa shughuli za ulinzi.

Mwandishi : Mohamed Dahman/AP

Mhariri. Yusuf Saumu