1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Tadic ashinda uchaguzi Serbia

4 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1ra

BELGRADE

Rais Boris Tadic wa Serbia amemshinda mpinzani wake Tomislav Nikolic katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais uliofanywa nchini humo siku ya Jumapili.Kamisheni ya Uchaguzi mjini Belgrade imesema,Tadic anaelemea kambi ya Magharibi amejinyakulia asilimia 51 ya kura na mzalendo Nikolic amepata asilimia 48.

Tadic anataka kuiingiza Serbia katika Umoja wa Ulaya na anaungwa mkono na umoja huo.Lakini msimamo wa Tadic kuhusu jimbo lake la kusini,Kosovo unatofautiana na ule wa nchi nyingi za Umoja wa Ulaya zinazounga mkono uhuru wa Kosovo.Jimbo hilo linatazamia kujitangazia uhuru wake kutoka Serbia katika kipindi cha majuma machache yajayo.