1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin aishutumu Marekani kwa njama ya kuuvuruga uchaguzi wa bunge

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTXe

Rais wa Urusi, Vladamir Putin, ameishutumu Marekani kwa kupania kuuvuruga uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Urusi.

Rais Putin, ambaye analazimika kuondoka madarakani mapema mwaka ujao kwa mujibu wa katiba, amesema serikali ya mjini Washington inabeba dhamana kwa uamuzi wa waangalizi wa uchaguzi kutoka shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya, OSCE, kuugomea uchaguzi wa bunge hapo terehe 2 mwezi ujao.

Ulaya imejiunga na Marekani kueleza wasiwasi wake juu ya ukandamizaji na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya maandamano ya upinzani yaliyofanywa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mmoja wa viongozi wa muungano wa upinzani nchini Urusi, Garry Kasparov, ni miongoni mwa madarzeni ya watu waliotiwa mbaroni na polisi.