1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Obama kuufanyia mabadiliko mfumo wa uchumi nchini Marekani.

18 Juni 2009

Mfumo huu mpya unalenga kuilinda Marekani kukumbwa na mzozo wa kuichumi sawa na ulio sasa katika siku za usoni.

https://p.dw.com/p/ISm5
Rais wa Marekani Barack Obama.Picha: AP

Rais wa marekani Barack Obama amependekeza kuufanyia mabadiliko makubwa mfumo wa uchumi wa marekani pamoja na njia ambazo zinaweza kuzuia mzozo mbaya wa kiuchumi kama ule uliopo sasa duniani kujirudia tena.

Waziri wa fedha nchini Marekani Timothy Geithner anatarajiwa kuwasilisha mpango wa mabadiliko ya mfumo wa uchumi wa Marekani katika bunge hii leo pamoja na kwenye kamati inayohusika na maswala ya fedha katika bunge la Marekani.

Mpango huo wa rais Obama una lengo la kuipa mamlaka benki kuu nchini Marekani, ili kusimamia masuala yote ya kifedha na kuunda mbinu ambazo zinaweza kuzuia kuwepo tena kwa vyanzo vilivyo sababisha kutokea kwa mzozo wa kiuchumi uliopo sasa.

Wadadisi wanasema kuwa mabadiliko hayo yaliyopendekezwa na rais Obama ni muhimu hasa kwa masoko yanayokabiliwa na matatizo lakini pia huenda yakawa vigumu kutekelezwa.

Akiuanzisha mpango huo jana jumatano rais Obama alisema kuwa hayo ndio mabadiliko makubwa zaidi tangu mwaka 1930, yaliyo na lengo la kuzuia kuporomoka kwa mifumo ya kifedha ambayo mara nyingi hutokana na kuwepo kwa madeni.

Hata hivyo kuna baadhi ya wanaoukosoa mpango huo wakisema kuwa, hautafanikiwa vile inayohitajika huku wengine wakisema kuwa serikali itakuwa na ushawishi mkubwa juu ya sekta za kibinafsi.

Kati ya mapendekezo kwenye mpango huo ni pamoja na kuipa benki kuu madaraka ya kuingilia kati mifumo ya uchumi ambayo inaonekana kuhatarisha uchumi ikiwemo ile ambayo haimiliki mabenki.

Flash-Galerie GM General Motors
Kampuni la General Motors lililofilisika nchini Marekani.Picha: picture alliance / landov

Hatua hizi ni muhimu na zinahitajika, lakini zinakosa mabadiliko makuu ambayo yangesaidia katika kutimiza malengo haya, alisema Douglas Elliot mwana uchumi mmoja katika taasisi moja nchini Marekani.

Mwana uchumi huyo alisema kuwa pia kunahitajiwa kufanyika mabadiliko katika makampuni makubwa, ambayo yanaweza kusababisha kuyumba kwa uchumi na pia na kuwalinda wananchi kiuchumi, matamshi ambayo pia yalitolewa na kundi linalowajumuisha wafanibiashara pamoja na wasomi lililobuniwa mwaka 2006.

Mpango huo unatajwa kulenga moja kwa moja masuala muhimu pamoja na mabadiliko makubwa na kuweka mikakati ya kukabiliana na masula yaliyochangia kutokea kwa mzozo uliopo sasa.

Hata hivo wengi wameukosoa mpango kuwa kuwa mkali, ambao huenda ukazuia uwekezaji katika mifumo ya uchumi. Wanasema kuwa mpango huo utalegeza huduma zinazotolewa na mifumo ya kuichumi na kutoa uishindani kati ya makampuni makubwa na yale ambayo bado ni madogo.

Hali kadhalika kuna wasi wasi, kwa wale wanaoutaja mpango huo kama ulio mkubwa mno, na huenda ukawa vigumu kuutekeleza na vile vile ukatoa hali ya kutokuwepo kwa utabiri katika siku za mbeleni kwenye masoko ya kifedha na katika badhii ya mifumo ya uchumi.

Mwandishi : Jason Nyakundi/AFP

Mhariri : Mohamed Abdul Rahman