1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Nicolas Sarkozy aahidi Ufaransa inamuunga mkono Mahmoud Abbas wa Palastina

30 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBn5

Paris:

Kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas amezungumzia haja ya kuitishwa uchaguzi katika ukanda wa Gaza chini ya ulinzi wa vikosi vya kimataifa.”Hiyo ndiyo njia pekee ya kuunusuru Umoja wa wapalastina” amesema rais Mahmoud Abbas baada ya mazungumzo pamoja na rais Nicolas Sarkozy mjini Paris.Nchi yake anasema rais Mahmoud Abbas inahitaji sio tuu usalama,bali pia matumaini mema.Rais Nicolas Sarkozy amemhakikishia rais Abbas uungaji mkono wa nchi yake.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Bernard Kouchner amesisitiza utawala wa ndani wa Palastina ndio “wawakilishi pekee halali wa Umma wa Palastina.”