Rais Musharraf kuzuru nchi 4 barani Ulaya
20 Januari 2008Matangazo
ISLAMABAD: Rais wa Pakistan Pervez Musharraf yupo njiani kuanza ziara ya mataifa 4 barani Ulaya.Ziara hiyo ya siku 8 nchini Ubeligiji,Ufaransa,Uswissi na Uingereza inafanywa wakati ambapo Pakistan inakabiliwa na ghasia na mivutano ya kisiasa.
Nchi za Ulaya zimeeleza wasi wasi kuhusu uchaguzi unaotazamiwa kufanywa nchini Pakistan.Uchaguzi huo uliahirishwa baada ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Benazir Bhutto kuuawa katika shambulizi la bomu hapo Desemba mwaka jana. Pakistan ni nchi pekee ya kiislamu inayodhibiti silaha za kinyuklia.