Rais Kikwete amteua Mwana-CUF kama mbunge
11 Februari 2010Matangazo
Bwana Ismail Jussa wa chama cha wananchi CUF, anaapishwa kesho kuwa mbunge katika bunge la muungano wa Tanzania, kufuatia hatua ya Rais wa nchi hiyo, mheshimwa Jakaya Kikwete kumteua. Josephat Charo amezungumza na Bwana Hamad Rashid, kiongozi wa upinzani katika bunge la muungano wa Tanzania, kuhusu uteuzi wa Bwana Jussa na kwanza kumuuliza ameupokea vipi uteuzi huo.
Mwandishi: Josephat Charo Mhariri: Mohamed Abdulrahman