1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kibaki autengua uteuzi wake,Kenya

Thelma Mwadzaya22 Februari 2011

Nchini Kenya,baada ya wiki kadhaa za vuta ni kuvute,Rais Mwai Kibaki ameutengua uteuzi wake wa maafisa wa ngazi za juu katika idara ya sheria.

https://p.dw.com/p/10M14
Rais wa Kenya Mwai Kibaki akiapishwa 2010 baada ya kuundwa katiba mpyaPicha: AP

Uteuzi huo ulifanyika mwezi uliopita na ulizua mitazamo na hisia tofauti katika serikali ya Kenya ya muungano wa Kitaifa.Rais Kibaki aliwateua Jaji Mkuu mpya,Mwanasheria Mkuu,Mwendesha mashtaka pamoja na Msimamizi wa Bajeti.Hata hivyo utata ulizuka baada ya Waziri Mkuu raila Odinga kusema kuwa hakuhusishwa katika shughuli hiyo,jambo lililosababisha mvutano.

Kenia Wahl Nairobi Flash-Galerie
Raia wa Kenya wakipiga foleni wakati wa uchaguzi uliopita .Picha: AP

Rais Kibaki alisisitiza kuwa kamwe hakuikiuka katiba na aliyatimiza majukumu yake kama anavyoruhusiwa.Hata hivyo itakumbukwa kuwa Spika wa Bunge la Kenya,Kenneth Marende,alisema kuwa uteuzi huo uliikiuka katiba.Mahakama Kuu iliyoko mjini Nairobi nayo pia iliuunga mkono mtazamo huo.