Rais wa Kenya Mwai Kibaki asema usalama wa raia ni muhimu na watafanya kila jitihada kuwalinda
Rais wa Kenya Mwai Kibaki
Rais wa Kenya, Mwai Kibaki amesema usalama utaimarishwa msimu huu wa sikukuu ya Krisamasi kufuatia mlipuko wa bomu lililotokea jana mjini Nairobi.
Kamishna wa polisi nchini Kenya, Mathew Iteere, amesema uchunguzi umeanza kubaini kama mlipuko uliowaua watu 3 na kuwajeruhi wengine wapatao 40 mjini Nairobi jana jioni, ni shambulio la kigaidi.
Mlipuko huo uliotokea kwenye basi moja la kuelekea Kampala, Uganda. Kamishna Iteere, hakuuleza mlipuko huo kuwa shambulio la kigaidi, lakini amesema umesababishwa na kifaa cha kulipuka kilichokuwa sehemu ya mzigo wa abiria. Bwana Iteere pia amesema uchunguzi umeanza kubaini waliohusika kufanya hujuma hiyo. Mwandishi wetu wa Nairobi, Alfred Kiti ametutumia taarifa ifuatayo.
Mwandishi: Alfred Kiti
Mhariri: Abdul-Rahman