1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Karzai atetea uteuzi wake wa mawaziri

Kabogo Grace Patricia21 Desemba 2009

Asema baraza hilo jipya la mawaziri litawajibika ipasavyo.

https://p.dw.com/p/L9ZG
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan.Picha: AP

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan ameahidi kuwa baraza lake jipya la mawaziri litawajibika kufuatia ukosoaji kuhusu rushwa katika serikali yake. Orodha rasmi ya majina 23 ya watu waliopendekezwa na Rais Karzai kuchukua nafasi za uwaziri iliwasilishwa katika bunge la nchi hiyo siku ya Jumamosi kwa ajili ya kuidhinishwa na itajadiliwa katika siku zijazo.

Rais Karzai amekuwa katika shinikizo kutoka mataifa ya Magharibi kuusafisha utawala wake kufuatia uchaguzi wa mwezi Agosti, mwaka huu kugubikwa na udanganyifu.

Wakati huo huo, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na viongozi wa Taliban wenye msimamo wa wastani nchini Afghanistan. Hatua hiyo inaonyesha mabadiliko ya sera za Ujerumani ambazo awali zilikuwa zinapinga kuhusiana na Taliban.