Rais Kagame azungumzia uhusiano kati ya Rwanda na Tanzania
2 Julai 2014Matangazo
Rais Paul Kagame ameyasema hayo mjini Kigali kwenye kikao na waandishi wa habari.Nchi za Rwanda na Tanzania zilikabiliwa na wakati mgumu kuanzia mwaka jana kutokana na kutofautiana kuhusu kundi la waasi wa kihutu la FDLR linaloendesha mambo yake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya utawala mjini Kigali.
Mwandishi wetu Sylivanus Kalemera kutoka Kigali ana ripoti zaidi. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Sylivanus Kalemera
Mhariri: Saumu Yusuf