1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Conte wa Guinea afariki.

Abdu Said Mtullya23 Desemba 2008

Rais Lansana Conte wa Guinea afariki dunia.

https://p.dw.com/p/GLiW
Rais Lansana Conte wa Guinea.Picha: AP Photo

Rais Lansana Conte wa Guinea amefariki dunia.

Spika wa bunge la nchi hiyo amefahamisha habari za kifo cha dikteta huyo alieitawala Guinea kwa muda wa miaka 24.

Conte aliekuwa na umri wa miaka 74 alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari na aliwahi kudodoswa na kansa ya damu.

Conte aliingia madarakani baada ya kuiangusha serikali mnamo mwaka 1984, bila ya damu kumwagika.

Waziri mkuu wa Guinea Ahmed Tidiane Soure ametangaza siku 40 za maombolezo ya kitaifa.

Waziri mkuu Soure amesema bendera zitapepea nusu mlingoti na taarifa juu ya maziko zitatolewaa baadae leo.

Dikteta Conte , aliekuwa mwanajeshi,alitumia jeshi kuimarisha mamlaka yake .Alitwaa mamlaka hayo kwa kuiangusha serikali mnamo mwaka 1984, wiki moja baada ya kifo cha rais wa kwanza wa Guinea Ahmed Sekou Toure.

Conte aliugua kwa muda mrefu.