Rais Chavez atishia kukatiza usafirishaji wa mafuta kwa Marekani
11 Februari 2008Matangazo
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez, ametishia kukatisha usafirishaji wa mafuta kwa Marekani baada ya kampuni kubwa ya kimarekani ya Exxon Mobil kushinda kuishawishi mahakama itoe amri ya kuzifungia mali za Venezuela za thamani ya dola bilioni 12.
Kampuni hiyo imewasilisha maombi katika mahakama za Marekani, Uingereza na Uholanzi kupinga hatua ya Venezuela kutaifisha visima vyake vya mafuta.
Rais Hugo Chavez ameishutumu Marekani kwa kushirikiana na kampuni hiyo kubwa ya mafuta duniani katika mashtaka hayo na kudai kwamba serikali ya mjini Washington inafanya vita vya kiuchumi dhidi ya Venezuela