1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush azitaka nchi za Kiarabu kuzitenga Iran na Syria

18 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E23Y

SHARM EL SHEIKH

Rais Goerge W Bush wa Marekani amezitolea mwito nchi za mashariki ya kati kutia juhudi za kutafuta amani ya kudumu kwenye eneo hilo.Akizungumza mbele ya jukwaa la kiuchumi duniani mjini Sharm El Sheikh nchini Misri rais Bush amesisitiza kwamba amani inaweza kupatikana kati ya Israel na Palestina ikiwa pande hizo mbili zitajitolea kuchukua hatua zinazostahili pamoja na Israel kufanya maamuzi magumu.Amesema anaamini ikiwa kutakuweko uongizi na ujasiri makubaliano ya amani yatafikiwa mwaka huu.''

Aidha katika hotuba hiyo ambayo imekamilisha ziara yake mashariki ya kati amesema nchi za kiarabu zinabidi kukubali kufuata demokrasia na kukabiliana na kundi la Hamas ambalo linadhiti ukanda wa Gaza.Pia amezungumzia suala la Lebanon na kuzishutumu Iran na Syria kwa kuchochea ghasia za hivi karibuni katika nchi hiyo kwa kudai kwamba nchi hizo zinawafadhili Hezbollah.Vilevile amezitolea mwito nchi za kiarabu kuizuia Iran isiendelee na mpango wake wa Nuklia kwa kusema kwamba nchi hiyo ina malengo ya kutengeneza sialaha za Kinukulia.Amesema Kuiachia nchi hiyo inayounga mkono ugaidi kutengeneza sialha za maangamizi itakuwa ni usaliti mkubwa dhidi ya kizazi kijacho,na kwa ajili ya amani ulimwengu lazima uizuie Iran isitengeneze silaha za Nuklia.Iran inasisitiza kwamba mpango wake wa Nuklia ni kwa malengo ya matumizi ya amani.