1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Madagascar wamchagua rais wao

25 Oktoba 2013

Raia wa Madagascar wanapiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo huku wengi wakiwa na matumaini ya ya kumalizika kwa mgongano kisiasa

https://p.dw.com/p/1A668
Picha: Rijasolo/AFP/Getty Images

Wapiga kura walipanga foleni mapema asubuhi tayari kuanza zoezi la kupiga kura katika vituo mbali mbali vilivyoandaliwa kupigiwa kura.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa majira ya saa 12 asubuhi kwa saa za Madagscar, huku kukiwa na wapiga kura 50 tu wakiwa wamepanga foleni katika kituo cha kupigia kura cha shule moja nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo

Huku serikali ya sasa ikitangaza leo kuwa ni siku ya mapumziko ili kuruhusu wananchi wengi zaidi kupiga kura, lakini kwa taifa kama Madagascar lenye umaskini wa kupindukia ambapo miongoni mwa watu wake wanapata kipato cha chini ya dola moja kwa siku, watu wengi wametumia nafasi hiyo kwenda kwenye biashara zao za kila siku, kufanya shuhguli zao mbali mbali na kutekeleza majukumu ya nyumbani

Hali hiyo itavunja matumaini ya Tume ya uchaguzi iliyotangaza kwamba zaidi ya watu milioni 7.8 wenye haki ya kupiga kura wamejiandikisha kupiga kura katika vituo milioni 20,000 vya kupigia kura

Kwa mujibu wa mpiga kura mmoja aliyefika kituoni kwake mapema asubuhi, Alain Yves matumaini yake ni kuona uchaguzi huo ukifanyika kwa amani na kwa maoni yake zoezi la kupiga kura hadi wakati huo lilikuwa linakwenda salama.

Wahlen in Madagaskar
Wagombea 33 kuwania kiti cha urais MadagascarPicha: RIJASOLO/AFP/Getty Images

Jumla ya wagombea 33 wanapigiwa kura katika kiti cha urais wakiwemo mawaziri wa zamani wa nchi hiyo , wanaplomasia, wachambuzi wa siasa na wasanii, ingawa ni wagombea sita tu wenye dalili za kushinda.

Uchaguzi wa Madagascar utamwondoa madarakani Andry Rajoelina ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa miaka minne na kumfanya aliyekuwa rais wa taifa hilo wakati huo Marc Ravalomanana kukimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini.

Wanasiasa wakongwe wazuiwa kugombea

Hata hivyo Tume ya uchaguzi nchini humo imewazuia kugombea tena urais, viongozi hao wakuu kisiasa,ili kuepusha mivutano ya kisiasa kuhujumu mchakato huo.

Uchaguzi huo unaleta matumaini kwa raia wa Madagascar kuwa utakuwa ni mwanzo mpya baada ya miaka minne ya kususiwa misaada na uwekezaji na kuyumbisha uchumi wa nchi hiyo ulioambatana na kuongezeka kwa umaskini

Kufuatia kuyumba huko nchi hiyo imekuwa ikifanya juhudi za kuvutia watalii na kuboresha rasilimali za mafuta, madini na nyingine.

Rais mpya atakiwa kuongeza ajira

Kwa mujibu wa raia wa nchi hiyo, Faly Randrianarivo ana matumaini kwamba rais mpya atakayechaguliwa atapanua wigo wa ajira, kupambana na umaskini na kuhakikisha elimu kwa wote kwa shule za msingi.

Armut in Madagaskar
Ni matumaini ya wengi kuwa baa la njaa litapungua miongoni mwa raiaPicha: picture-alliance/AP Photo

Mmoja wa waangalizi katika uchaguzi huo, Madan Dulloo amesema anaamini hakutakuwa na wizi wa kura katika vituo vya uchaguzi .

Hata hivyo baadhi ya wapiga kura wameonyesha wasi wasi wao kwamba matokeo ya uchaguzi yanaweza yasiwe huru na haki na kusababisha ghasia kubwa zaidi

Mwandishi: Flora Nzema/APE/RTRE/AFPE
Mhariri: Suamu Yusuph Mwasimba