1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pyongyang.Korea ya Kaskazini yasema vikwazo dhidi yake ni tangazo la vita.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1q

Korea ya kaskazini imesema kuwa vikwazo ilivyowekewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni “Tangazo la vita“ na imeapa kukabiliana na nchi yoyote itakayo vitekeleza.

Haya yamekuja wakati vyanzo vya habari vya Marekani, Korea ya Kusini na Japan, vikidai kuwa taifa hilo la Kikomunisti linajitayarisha kufanya jaribio la pili la bomu la nyuklia, baada ya wapelelezi wa Marekani kuwa na harakati karibu na sehemu iliyofanywa jaribio la awali.

Kufuatia mazungumzo huko Korea ya Kusini, mjumbe wa Marekani Christopher Hill amesema, jaribio la pili linaweza kuangaliwa na Marekani kama kitendo cha uadui.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bibi Condoleezza, anaetazamiwa kuitembelea Korea ya Kusini, Japan na China, ameionya Iran kwamba lazima izingatie vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea ya Kaskazini kuwa ni kama mfano.