PYONGYANG: Mamia ya watu wauwawa kwenye mafuriko | Habari za Ulimwengu | DW | 14.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PYONGYANG: Mamia ya watu wauwawa kwenye mafuriko

Vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini vimeripoti kwamba mamia kadhaa ya raia wameuwawa kufuatia mafuriko nchini humo.

Ripoti za awali zinasema nyumba zaidi ya 30,000 zimeharibiwa. Daraja na reli pia zimeharibiwa kufuatia mafuriko ya wiki nzima nchini humo.

Eneo lililoathirika zaidi ni mkoa wa Kangwon unaopatikana katika eneo la mpaka wa kusini wa Korea Kaskazini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com