PYONGYANG: Korea ya Kaskazini itahifadhi uwezo wa kujikinga | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PYONGYANG: Korea ya Kaskazini itahifadhi uwezo wa kujikinga

Korea ya Kaskazini imesema itabakia na mpango wake wa kukaa tayari kwa vita,ikiwa na hofu kuwa itashambuliwa na Marekani.Vyombo vya habari vya serikali vimesema kuwa katika barua iliyopelekwa kwa kiongozi Kim Jong-Il kuadhimisha miaka 65 tangu kuzaliwa kwake,chama cha kikomunisti cha nchi hiyo,serikali,jeshi na wananchi wameapa kufuata mwongozo wake kujenga taifa la kijamaa lililo imara.Siku ya Jumanne,mjini Beijing Korea ya Kaskazini katika majadiliano pamoja na Marekani na nchi nne zingine ilikubali kusitisha mradi wake wa kinyuklia na badala yake itapewa misaada tofauti.Makubaliano hayo pia yanatoa wito kwa Marekani kuanzisha majadiliano ya pande mbili pamoja na Pyongyang kwa azma ya kutenzua migogoro iliyopo kati yao na zisonge mbele kuelekea uhusiano kamili wa kibalozi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com