Putin ateua baraza la mawaziri | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.05.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Putin ateua baraza la mawaziri

Rais wa Urusi Vladimir Putin amelitaja baraza lake jipya la mawaziri na kuwatahadharisha aliowateua kwamba wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao japokuwa dunia ina hali mbaya ya kiuchumi.

Rais wa Urusi Vladmir Putin akiwa na baraza lake la mawaziri

Rais wa Urusi Vladmir Putin akiwa na baraza lake la mawaziri

Mawaziri waliomo katika baraza jipya na ambao walikuwemo katika serikali ya mtangulizi wake Dmitry Medvedev aliyechaguliwa uwaziri mkuu ni waziri wa ulinzi na waziri wa mambo ya nje tu huku wizara nyingine zikijazwa na sura mpya tu.

Waziri wa mambo ya nje ni Segey Lavrov, huku waziri wa ulinzi ni Anatoly Sedyukov na waziri wa fedha ni Anton Siluanov, la kushangaza wengi Rais Putin amemteua naibu waziri mkuu Igor Shuvalov japokuwa ana tuhuma za uwekezaji wake kadhaa na utajiri mwingi .

Baraza jipya la mawaziri la Urusi

Baraza jipya la mawaziri la Urusi

Baadhi ya wizara zilizopata mawaziri wapya ni pamoja na wizara ya afya, wizara ya elimu na wizara ya mambo ya ndani.

Waziri wa mambo ya ndani aliyepita alikumbwa na kashfa za utesaji wa watu na udhalilishaji uliofanywa na polisi wa nchi hiyo amewekwa kando na wizara hiyo amekabidhiwa aliyekuwa mkuu wa polisi wa Mosco Vladimir Kolokoltsev.

Waziri mwingine aliyekumbwa na kashfa ni kutoka Wizara ya afya ambapo kulikuwa na tuhuma za mipango mibaya katika bima za tiba. Nafasi yake amepewa naibu wake Veronika Skvortsova. Wizara ya elimu amekabidhiwa Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mosco Dmitry Livanov

Hali ya uchumi kupanda

Rais Putin mwenye umri wa Miaka 59 ambaye atasherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 60 oktoba mwaka huu akiwa Rais wa Urusi anaonekana kuwa na nia ya kukuza uchumi wa taifa hilo na kukaribisha mawazo mapya kwani amemteua mpinzani wake kiuchumi Andrei Belousov na kawa waziri wa uchumi.

Akilitazama jambo hilo Germany Gref aliyewahi kuwa waziri wa uchumi na mtaalamu wa masuala ya kibenki anasema tangu wakati wa kampeni Rais Putini alionyesha dalili za kuinua uchumi wa Urusi.

Rais Vladimir Putin na Jose-Manuel Barroso

Rais Vladimir Putin na Jose-Manuel Barroso

lakini mpaka Robo ya mwaka huu hali ya uchumi imeonekana kukua kwa asilimia 4.9 tu ambapo hali inadaiwa kutokana na fedha nyingine kutumika vibaya katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo uliomuweweka madarakani Rais Putin.

Wakati wa matayarisho ya uchaguzi uliomuweka madarakani Rais Putin kulikuwa na maandamano makubwa kwa madai kuwa ungekuwa na udanganyifu kama ule wa uchaguzi wa Bunge lakini uchaguzi ulifanyika huku waandamanaji hao wakikamatwa.

Mwandishi:Adeladius MakwegaDPAE/RTRE/APE

Mhariri: Yusuf Saumu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com