1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin aonya dhidi ya kutegwa kinga ya makombora ya Marekani nchini Poland na katika jamhuri ya Tcheki

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GJ

Moscow:

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani,Condoleezza Rice na mwenzake wa ulinzi Robert Gates wako ziarani mjini Moscow kwa mazungumzo pamoja na mawaziri wenzao wa Urusi.Mazungumzo haya ya leo yatahusu miongoni mwa mengineyo,mpango wa Marekani wa kutega mtambo wa kinga dhidi ya makombora katika jamahuri ya Poland na Tcheki,pamoja pia na mradi wa kinuklea wa Iran. Vladimir Putin ameitahadharisha Marekani dhidi ya kuendeleza kwa kila hali mpango huo.Rais Putin amewaambia mawaziri hao wa Marekani tunanukuu:

“Nnataka kukumbusha tuu kwamba sisi tunategemea kwamba hamtotekeleza kwa nguvu makubaliano yaliyofikiwa awali pamoja na mataifa ya Ulaya ya mashariki.Tunaweza kuafikiana siku moja mtambo wa kinga dhidi ya makombora ujengwe mwezini.Lakini kabla ya hayo kufikiwa,itakua vyema kama makubaliano haya yaliyoko hayatapuuzwa.”

Mazungumzo hayo yanahusu pia makubaliano kadhaa yaliyofikiwa wakati wa enzi za vita baridi.Rais Vladimir Putin ameuambia ujumbe wa Marekani,Urusi isingependelea kuendeleza makubaliano ya mwaka 1987 kuhusu makombora ya kinuklea ya masafa ya kati,ila kama yatazijumuisha nchi nyengine pia.Urusi imeshazigutua nchi za magharibi iliposema inataka kujitoa katika makubaliano mengine yaliyofikiwa katika enzi za vita baridi:makubaliano ya silaha zisizo za kinuklea.