1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRISTINA : Leo ni uchaguzi wa bunge Kosovo

17 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImF

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa nchini Kosovo leo hii kuichaguwa serikali huku kukiwa na hali ya mashaka juu ya hatima ya jimbo hilo .

Kosovo ambayo imekuwa ikiongozwa chini ya himaya ya Umoja wa Mataifa tokea mwaka 1999 bado ingali ni sehemu ya Serbia.Watu walio wengi katika jimbo hilo wa asili ya Albania wakiungwa mkono na Marekani wanatumai uchaguzi huo wa leo utaanzisha serikali ambayo italiongoza jimbo hilo la Serbia kuelekea kwenye uhuru.Hata hivyo Waserbia katika jimbo hilo na serikali yao ya Belgrade pamoja na Urusi wanapinga mpango huo. Serikali ya Serbia imewashauri Waserbia wa Kosovo kuususia uchaguzi huo.

Viti 120 vya bunge vinawaniwa katika uchaguzi huo ,100 vikiwa vimetengwa kwa vyama vinavyowakilisha Waalbania wenye kupendelea uhuru.

Kikosi cha wanajeshi 16,000 wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO kimeimarishwa kwa kuongezewa wanajeshi kadhaa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.