1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRAGUE: Bush awasili Jamuhuri ya Czech

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuk

Rais George Bush wa Marekani amewasili katika Jamuhuri ya Czech akiwa katika ziara ya siku nane barani ulaya.

Bush anatarajiwa kukutana na rais Vaclav Klaus na waziri wake mkuu Mirek Topolanek katika mji mkuu wa Prague.

Viongozi hao wanaunga mkono mpango wa rais Bush wa kuwekeza makombora ya ulinzi katika Jamuhuri ya Czech na Poland.

Mpango huo unapingwa vikali na rais Vladmir Puttin wa Urusi ambae ametishia kuwa iwapo Marekani itatekeleza mpango wake huo basi Urusi italazimika kuelekeza baadhi ya makombora yake katika nchi za ulaya.

Bush na Puttin watafanya mazungumzo ya pande mbili pembezoni mwa mkutano wa kilele wa G8 katika mji wa pwani ya Baltic wa Heiligendamm nchini Ujerumani baadae wiki hii.