POTSDAM:Mawaziri wakutana kutayarisha mkutano mkuu wa nchi tajiri | Habari za Ulimwengu | DW | 18.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

POTSDAM:Mawaziri wakutana kutayarisha mkutano mkuu wa nchi tajiri

Mawaziri wa fedha kutoka nchi nane tajiri duniani wanakutana katika mji wa Potsdam mashariki mwa Ujerumani kujadili njia za kuleta uengemavu katika masoko ya fedha.

Mawaziri hao wanakutana wakati ambapo zimebakia siku chache kabla ya mkutano mkuu wa viongozi wa nchi tajiri nane duniani utakaofanyika hapa nchini Ujerumani.Mawaziri hao pia wanazungumzia juu ya misaada kwa nchi zinazoendelea.

Wajumbe kutoka nchi kadhaa za Afrika ikiwa pamoja na Afrika Kusini pia wanahudhuria mkutano huo wa mjini Potsdam.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com