1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT - OF SPAIN : Mtuhumiwa ajisalimisha

6 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuS

Mtuhumiwa wa nne katika madai ya njama ya kuushambulia uwanja wa ndege wa New York wa John F.Kennedy amejisalimisha nchini Trinidad.

Abdel Nur amejisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi nje ya mji mkuu wa Port of Spain.Raia huyo wa Guyana anatuhumiwa kutaka msaada wa njama hiyo kutoka kwa kiongozi wa kundi la msimamo mkali la Kiislam nchini Trinidad.

Serikali inawashikilia watuhumiwa wawili katika njama hiyo ya New York ambao wanapinga kupelekwa nchini Marekani.