PORT HARCOURT:Mtoto wa kiume atekwa kusini mwa nchi | Habari za Ulimwengu | DW | 12.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PORT HARCOURT:Mtoto wa kiume atekwa kusini mwa nchi

Mtoto mmoja wa kiume raia wa Nigeria aliye na umri wa miaka mitatu ametekwa katika eneo la kusini mwa nchi.Kwa mujibu wa polisi Irejua Barasua,maafisa wa usalama wananachunguza aliyemteka mwanawe Eze Francis Amadi kiongozi wa kitamaduni katika eneo hilo.Wapiganaji wawili walimkamata mtotto huyo alipokuwa akielekea shuleni naye dereva wa gari alimokuwa akisafiria anahojiwa na polisi.

Huyo ni mtotto wa nne kutekwa katika kipindi cha takriban miezi miwili kwenye eneo la mafuta mengi ambalo limekabiliwa na visa vya utekaji mwingi mwaka huu.Zaidi ya raia 150 wa kigeni akiwemo mtotto mdogo na mwanamke mmoja wametekwa wakiwemo pia raia kadhaa wa Nigeria.Baadhi ya makundi hayo wanapigania uhuru wa kisiasa vilevile kunufaishwa na biashara ya mafuta katika eneo hilo lililo na umaskini mkubwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com