1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wafyetua risasi hewani Ukanda wa Magharibi

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUGJ

Polisi wanaomuunga mkono Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas,wamefyetua risasi hewani na wamewatandika waandamanaji katika mji wa Ukanda wa Magharibi,Hebron.Mashahidi wamesema,ghasia zilizuka pale waandamanaji walipowarushia mawe polisi,wakati wa mazishi ya mtu alieuawa siku ya Jumanne kwenye maandamano ya kupinga mkutano wa amani ya Mashariki ya Kati uliosimamiwa na Marekani.Wauguzi pia wamesema si chini ya watu darzeni mbili walijeruhiwa katika mapambano hayo.