PNOM PHEN: Kesi ya mauaji ya halaiki yaanza kusikilizwa | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PNOM PHEN: Kesi ya mauaji ya halaiki yaanza kusikilizwa

Tume ya kuchunguza mauajiy a halaiki nchini Cambodia ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kwa mara ya kwanza imeanza kusikiliza kesi ya mshukiwa wa Khmer Rouge baada ya miezi kadhaa ya migogoro.

Mshukiwa huyo, Kang Kek Ieu, anayejulikana pia kama Comrade Duch, aliongoza gereza la Tuol Sleng huko Phnom Penh wakati wa utawala wa kikatili wa serikali katika miaka ya 1970.

Inadaiwa alisimamia mateso na mauaji ya watu 16,000, wakiwemo wanaume, wanawake na watoto. Dush anapiga kuzuiliwa kwake. Kusikiliwa kwa kesi hiyo kunaonekana na wengi kama mtihani mgumu kwa tume hiyo na kunafanyika siku chache baada ya kongozi wa Khmer Rouge, Khie Samphan, kukamatwa na kushtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Inakadiriwa watu zaidi ya milioni moja waliuwawa wakati wa utawala wa Khmer Rouge kati ya mwaka wa 1975 na 1979.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com