PHUKET: Ajali ya ndege imeuwa 87 nchini Thailand | Habari za Ulimwengu | DW | 16.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PHUKET: Ajali ya ndege imeuwa 87 nchini Thailand

Hadi watu 87 wamepoteza maisha yao katika ajali ya ndege iliyotokea katika kisiwa cha mapumziko cha Phuket,nchini Thailand.Ndege ya shirika la Thailand la “One-Two-Go“ linalouza tikti za bei ya nafuu,ilikuwa na abiria 123 na wafanyakazi 5. Waziri wa Afya wa Thailand,Mogkol Na Songkhla amesema,watu 43 wamenusurika.Idadi kubwa ya abiria katika ndege hiyo iliyotokea Bangkok, walikuwa raia wa kigeni.

Mashahidi wamesema,ndege hiyo ilianguka katika hali mbaya ya hewa na ikapasuka.Baadae ikateleza kwenye njia ya kutua na ikajibamiza kwenye ukuta ulio kando ya barabara na ikashika moto.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com