PESHAWAR: Mshambulizi ajibamiza kwenye msafara wa majeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 15.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PESHAWAR: Mshambulizi ajibamiza kwenye msafara wa majeshi

Nchini Pakistan,shambulizi la bomu lililolenga msafara wa kijeshi limeua si chini ya wanajeshi na raia 14,katika mji wa Matta,karibu na mpaka wa Afghanistan.Kama 40 wengine pia walijeruhiwa katika shambulizi hilo jipya,lililotokea siku moja baada ya wanajeshi 24 kuuawa katika shambulizi la kujitolea muhanga ambalo pia lililenga msafara wa kijeshi.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya Pakistan,huenda ikawa kuna uhusiano kati ya mashambulizi hayo na hatua iliyochukuliwa na serikali kuuvamia Msiskiti Mwekundu wenye itikadi kali,mjini Islamabad,juma lililopita.Baada ya uvamizi huo uliosababisha zaidi ya vifo 100,Rais Pervez Musharraf wa Pakistan alisambaza maelfu ya wanajeshi katika maeneo yenye wasiwasi kwa azma ya kuzuia machafuko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com