1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pervez Musharraf kuapishwa rais kwa awamu ya pili

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUG2

Mawaziri wa zamani wa Pakistan,Benazir Bhutto na Nawaz Sharif wamekaribisha kujiuzulu kwa Pervez Musharraf kama mkuu wa majeshi.Musharraf katika sherehe iliyofanywa leo hii mjini Rawalpindi, alijiuzulu kama mkuu wa majeshi ili aweze kuapishwa kama rais,kwa awamu ya pili ya miaka mitano.

Musharraf alienyakua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 1999 bila ya umwagaji wa damu,ataapishwa siku ya Alkhamisi kama rais wa kiraia.Jemadari Ashfaq Parvez Kiyani amekabidhiwa wadhifa wa mkuu wa majeshi.