1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pep anaondoka Bayern au anabaki?

18 Desemba 2015

Bayern Munich imerefusha mikataba ya Thomas Mueller, Jerome Boateng na Javi Martinez hadi mwaka wa 2021 huku Xabi Alonso akiongezwa mwaka mmoja kwa mkataba wake

https://p.dw.com/p/1HQ5L
Trainer Pep Guardiola Bundesliga FC Bayern München
Picha: picture-alliance/dpa/Andreas Gebert

Huku kukiwa na uvumi kuhusu kocha Pep Guardiola na uwezekano wa yeye kuhamia ligi Kuu ya Kandanda ya England mwishoni mwa msimu huu, hatua hiyo ya kurefushwa mikataba ya wachezaji hao ni ishara ya nguvu za Bayern.

Mshambuliaji Thomas Mueller ambaye mkataba wake wa awali ulistahili kukamilika mwaka wa 2019, alikuwa akiwindwa sana na vilabu vikuu barani Ulaya.

Guardiola amesalia kimya kuhusu hatima yake huku klabu hiyo ikiwa na hamu ya kuurefusha mkataba wake. Bayern wamesema watatoa tangazo lao kabla ya mwishoni mwa mwaka huu.

Uvumi wa Guardiola kuondoka umeshika kasi, huku Carlo Ancelotti akiwa tayari amedokezwa kuwa mrithi wake katika klabu hiyo kuu ya Ujerumani.

Ancelotti anaweza kupewa nafasi maana ana tajriba kubwa. Amewahi kushinda mataji matatu ya Chapions League akiwa na AC Milan, mwaka wa 2003 na 2007 na Real Madrid mwaka wa 2014 wakati aliizaba Bayern mwaka huo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu