PASHAWAR:Mauaji zaidi huko Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 04.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PASHAWAR:Mauaji zaidi huko Pakistan

Watu sita wameuawa na wengine 31 wamejeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika kituo cha basi kilichokuwa na watu wengi huko kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Msemaji wa Polisi katika jimbo la Pashawar amesema kuwa mshambuliaji huyo alijilipua ndani ya gari alilokuwa akiendesha mara baada ya kufika kwenye kituo hicho cha basi kilichokuwa kimejaa watu.

Katika shambulizi lingine huko huko Pakistan, wanamgambo wanaoliunga mkono kundi la Taliban waliwafyatuilia risasi na kuwaua askari wanne kwenye kituo cha ukaguzi katika jimbo la Waziristan.Polisi walifanikiwa nao kuwauawa wanamgambo kumi.

Wakati huo huo kiongozi wa upinzani nchini Pakistan Javed Hashmi ameachiliwa hii leo kutoka gerezani alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka minne.

Mamia ya wafuasi wake walimlaki kiongozi huyo mjini Lahore mara baada ya kuachiwa ambapo aliahidi kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Rais Perves Musharraf.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com