1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS:Wafaransa wapiga kura huku usalama ukiimarishwa kote

Wafaransa wanapiga kura katika uchaguzi wa duru ya pili ya kinyang’anyiro cha urais kati ya Nicolas Sarkozy wa chama tawala cha kihafidhina cha UMP na Segolene Royal wa chama cha Kisosholisti.

Kura za maoni za hivi karibuni zinaonyesha kuwa bwana Sarkozy wa chama tawala anaongoza kwa asilimia 10 ya pointi mbele ya bibi Segolene Royal.

Kufikia wakati wa adhuhuri ya leo kiasi cha asilimia 35 ya wapiga kura walikuwa wameshapiga kura hii ikiwa ni idadi kubwa ya watu kuwahi kujitokeza mapema kiasi hicho katika historia ya miaka 30 ya uchaguzi nchini Ufaransa.

Bibi Segolene Royal siku ya ijumaa alionya endapo Sarkozy atashinda uchaguzi huu kutatokea vurugu nchini Ufaransa lakini hadi sasa maofisa wanasema hakujajitokeza dalili za kutokea fujo hizo.

Maelfu ya polisi wa kukabiliana na fujo na wanajeshi wamekwekwa tayari kote nchini kupambana na ghasia zozote zitakazozuka endapo bwana Sarkozy atatangazwa mshindi.

Mshindi kwenye kinyang’anyiro hiki cha urais atajulikana muda usio mrefu jioni hii.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com