PARIS:serikali mpya kuundwa nchini Ufaransa
19 Juni 2007Matangazo
Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amemwagiza waziri wake mkuu bwana Francois Fillon kuunda serikali mpya baada ya chama cha kihafidhina cha rais huyo kushinda katika uchaguzi wa bunge mwishoni mwa wiki iiyopita. Chama cha rais Sarkozy kilishinda kwa kupata viti 314 katika bunge lenye viti 577.
Rais huyo amesema atatumia fursa inayotokana na ushindi huo kutekeleza mageuzi aliyowaahidi wananchi wake, ikiwa pamoja na kuweka sheria ngumu za uhamiaji, kupunguza kodi na kurekebisha mfumo wa afya uliolemewa na deni.