1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Mashtaka mapya kwa Carlos the Jackal

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4p

Gaidi lililotikisa dunia, Carlos the Jackal anakabiliwa na mashtaka mengine kuhusiana na ulipuaji wa mabomu katika miaka ya 80 uliyopelekea watu 11 kuawa.

Carlos ambaye jina lake ni Ilich Ramirez Sanchez tayari anatumikia kifungo cha maisha katika magereza nchini Ufaransa kwa tuhuma za mauaji ya majasusi wawili wa Ufaransa mwaka 1975.

Jaji mwanaharakati dhidi ya ugaidi Jean Louis Bruguire ametaka kufunguliwa kwa mashtaka mapya.