1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Paris.Basi lachomwa moto kufuatia ghasia nchini Ufaransa.

Kumetokea ghasia nyengine katika vitongoji viwili vya Paris usiku wa kuamkia leo zilizosababishwa na kundi la vijana waliochoma moto basi.

Abiria wote na dereva waliokuwemo katika basi hilo, walifanikiwa kutoka bila ya athari yoyote.

Kiasi cha vijana 50 walizirushia mawe gari katika kitongoji cha Grigny.

Mashambulio haya ya hivi sasa yamekuja baada ya wiki kadhaa za machafuko kiasi cha mwaka mmoja uliopita, ambayo yalipelekea magari elfu kumi na majumba katika miji 300 nchini Ufaransa kuharibiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com