1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Waziri wa Mambo ya ndani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy ateuliwa rasmi kuwa mgombea urais.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCae

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, leo ametangazwa rasmi kuwa mgombea wa urais wa chama kinachotawala cha Union for a Popular Movement (UMP).

Wanachama wa chama hicho walimteua Nicolas Sarkozy kwa kumpigia kura kupitia mtandao ingawa alikuwa na uhakika wa kuteuliwa kwani hakuwa na mpinzani.

Shughuli ya kumtangaza rasmi Nicolas Sarkozy kuwa mgombea wa urais imefanyika kwenye kikao cha chama hicho kilichoandaliwa mjini Paris.

Rais Jacque Chirac ambaye hakuhudhuria kikao hicho, hajatangaza iwapo atagombea kipindi cha tatu kwenye uchaguzi wa mwezi Aprili.

Mgombea wa urais wa chama cha kishosolisti ni Bibi Segolene Royal.