PARIS: Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, ziarani Ufaransa. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS: Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, ziarani Ufaransa.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair yumo ziarani nchini Ufaransa ambako ameshauriana na Rais anayeondoka, Jacques Chirac na Rais-mteule, Nicolas Sarkozy.

Mkutano huo ndio wa mwisho rasmi kati ya Tony Blair na Jacques Chirac ambaye juma lijalo atamkabidhi urais Nicolas Sarkozy.

Tony Blair ameshatangaza atang’atuka mnamo tarehe 27 mwezi ujao.

Blair alitangaza hayo saa chache baada ya kumuidhinisha Waziri wa Fedha, Gordon Brown, kuurithi uongozi wa chama tawala cha Leba na pia wadhifa wa waziri mkuu.

Gordon Brown tayari amezindua rasmi harakati zake za kuwania uongozi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com