1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Watu 24 wafariki katika ajali ya basi

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgA

Watu wasiopungua 24 wamefariki katika ajali ya basi iliyotokea katika mji wa Grenoble,kusini-mashariki ya Ufaransa.Wengine 20 walijeruhiwa, baadhi yao wakiwa mahututi.Basi hilo lilikuwa na kama waumini 50 wa Kikatoliki kutoka Poland na liliangukia bondeni,lilipokuwa likipita kwenye barabara ya mteremko mkali,katika Milima ya Alps nchini Ufaransa.Baada ya kubomoa kizuizi na kuaunguka mita 15 chini kwenye ukingo wa mto,basi lilishika moto.