PARIS: Waandishi wa habari 81 wauwawa mwaka wa 2006
1 Januari 2007Matangazo
Mwaka wa 2006 umekuwa mwaka mgumu kwa waandishi wa habari katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Shirika linalotetea uhuru wa vyombo vya habari, Reporters Without Borders, limesema mjini Paris Ufaransa kwamba waandishi wa habari 81 na wafanyakazi wengine 32 wa vyombo vya habari waliuwawa kwa sababu ya kazi yao.
Shirika hilo limesema idadi hiyo ni kubwa zaidi tangu mwaka wa 1994 ambapo waandishi habari wengi waliuwawa wakati wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda.