1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Ségolène Royal kukiwakilisha chama cha kisoshialisti kwenye uchaguzi wa urais mwakani nchini Ufaransa

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrx

Bibi Ségolène Royal kutoka chama cha kisoshialisti nchini Ufaransa, amepiga hatua mbele kuelekea kiti cha urais nchini Ufaransa baada ya kuchaguliwa kukiwakilisha chama katika uchaguzi wa urais mwaka ujao. Bibi Ségolène Royal, ambae ni waziri wa zamani wa mazingira, amepata asili mia 60 ya kura dhidi ya wagombea wengine ikiwa ni pamoja na waziri wa zamani wa fedha Dominique Strauss-Kahn ambae amepata asili mia 20 na waziri mkuu wa zamani Laurent Fabius ambae amepata asili mia 18.

Baada ya kutangazwa matokeo ya kura hiyo, bibi Ségolène Royal, alisema hatua hiyo imemuimarisha kisiasa:

´´Kama alivyosema marehemu Francois Mitterand, ukiwa kwenye mtihani, aidha utakuzamisha au utakuinua. Sasa, nimeinuka´´.

Kulingana na kura za maoni, Bibi Ségolène Royal ndie mtu anayeweza kumshinda mgombea kiti cha urais kutoka chama cha konsevative cha rais Jacques Chirac, Nicolas Sarkozy, ambae ni waziri ma mambo ya ndani.