PARIS : Mgomo wa reli wapamba moto | Habari za Ulimwengu | DW | 17.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS : Mgomo wa reli wapamba moto

Mgomo wa reli nchini Ufaransa umezidi kupamba moto katika siku yake ya nne huku treni zinazofanya kazi zikizidi kuwa chache.

Mgomo huo umeitishwa kupinga mpango wa mageuzi ya malipo ya uzeeni wa Rais Nicolas Sarkozy.Wafanyakazi wa reli wameamuwa hapo jana kuendelea na mgomo huo hadi Jumatatu licha ya wito wa chama kimoja cha wafanyakazi chenye msimamo wa wastani kuwataka warudi kazini na kuwepo kwa uwezekano wa mazungumzo na shirika la reli la taifa SNCF.

Shirika hilo limependekeza kwa vyama vya wafanyakazi hao utaratibu wa kuangalia malalamiko yao ambapo mkutano wa kwanza ukitarajiwa kufanyika hapo tarehe 21 mwezi wa Novemba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com