1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Kongamano la kimatifa kupinga adhabu ya kifo

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCW0

Kongamano la tatu la kimataifa dhidi ya adhabu ya kifo limefunguliwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.Katika hotuba ya kufungua kongamano hilo,rais Jacques Chirac wa Ufaransa amesema anafurahishwa kuona upinzani dhidi ya adhabu ya kifo ukiongezeka wakati ambapo katika sehemu mbali mbali duniani bado adhabu ya kifo yaendelea kutumiwa.Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambae hivi sasa ameshika wadhifa wa urais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya,katika risala yake amesema,ugaidi pia unaweza kupigwa vita kwa kuhifadhi kwa dhati misingi ya maadili.Hadi Jumamosi,kiasi ya wajumbe 1,000 wanaohudhuria kongamano hilo,wanashauriana kuhusu miito ya kupiga marufuku adhabu ya kifo,ambayo bado huendelea kutumika katika nchi 69.