PARIS: Chirac asisitiza umuhimu wa kuzuia muongezeko wa joto duniani | Habari za Ulimwengu | DW | 03.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS: Chirac asisitiza umuhimu wa kuzuia muongezeko wa joto duniani

Waziri Mkuu wa Israel, Ehud Olmert

Waziri Mkuu wa Israel, Ehud Olmert

Rais Jacques Chirac wa Ufaransa ametoa wito wa kuunda Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.Alitamka hayo mjini Paris wakati wa kufunga mkutano uliotoa ripoti inayotia hofu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani.Chirac amesema,kuna haja ya kuwa na shirika maalum litakalorithi “Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa“ kupambana na tatizo la muongezeko wa joto la ardhi pamoja na uharibifu mwingine wa sayari yetu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com