1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa mpya huyu hapa

13 Machi 2013

Jorge Mario Bergoglio kutoka Argentina ndiye Baba Mtakatifu mpya atakayeliongoza kanisa katoliki baada ya kujulishwa hapo jana usiku kwa ulimwengu. Kuanzia sasa anafahamika kama Baba Mtakatifu Francisco wa Kwanza.

https://p.dw.com/p/17wyH
VATICAN CITY, VATICAN - MARCH 13: Newly elected Pope Francis I appears on the central balcony of St Peter's Basilica on March 13, 2013 in Vatican City, Vatican. Argentinian Cardinal Jorge Mario Bergoglio was elected as the 266th Pontiff and will lead the world's 1.2 billion Catholics. (Photo by Peter Macdiarmid/Getty Images)
Jorge Bergoglio ni Papa mpyaPicha: Getty Images

Baba Mtakatifu Francisco wa Kwanza mwenye umri wa miaka 76 alichaguliwa hapo jana na makadinali 115 baada ya siku mbili ya uchaguzi na anamrithi Benedict wa kumi na sita mabaye alijiuzulu mwezi uliopita. Papa huyo ni wa 266 tangu kanisa hilo kuanzishwa miaka elfu mbili iliyopita na wa kwanza kuchaguliwa kutoka Amerika ya Kusini na wa kwanza kutotoka barani Ulaya tangu karne ya kumi na nane.

Franisco ni Jina kwanza kutumika

Jina lake Francisco pia ndiyo mara ya kwanza kutumika na papa. Amekuwa kadinali wa Argentina tangu mwaka 1988 na amekuwa ktaika mstari wa mbele katika usimamizi wa masuala ya kiutawala wa kanisa hilo na hivyo kudhihirisha kuwa ataweza kutekeleza majukumu ya kuwa papa vyema.

VATICAN CITY, VATICAN - MARCH 13: Newly elected Pope Francis I appears on the central balcony of St Peter's Basilica on March 13, 2013 in Vatican City, Vatican. Argentinian Cardinal Jorge Mario Bergoglio was elected as the 266th Pontiff and will lead the world's 1.2 billion Catholics. (Photo by Peter Macdiarmid/Getty Images)
Papa mpya Jorge Bergoglio akiwa kati makadinali wenginePicha: Getty Images

Mwaka 2005 inasemekana aliibuka wa pili kwa wingi wa kura baada ya Benedict wa 16. Papa Francisco wa kwanza amekuwa akijishughulisha sana kuwafunza na kuwalea makasisi katika eneo la Amerika ya kusini ambalo lina waumini wengi zaidi  ya kote ulimwenguni na hilo kumfanya kuonekana kumweka katika hali nzuri kuongoza kanisa Katoliki, na amelibadili sura kanisa hilo katika eneo hilo la kihafidhina.

Aomba baraka za waumini

Katika hotuba yake ya kwanza katika ubaraza wa ghorofa ya Basilica aliwaomba waumini kote duniani wa nia na kheri njema  wamuombee baraka na pia alimuombea Papa anayeondoka Benedikto wa Kumi na Sita.

Faithful cheer as white smoke rises from the chimney above the Sistine Chapel, indicating a new pope has been elected at the Vatican, March 13, 2013. White smoke rose from the Sistine Chapel and the bells of St. Peter's Basilica rang out on Wednesday, signaling that Roman Catholic cardinals had ended their conclave and elected a pope to succeed Benedict XVI. REUTERS/Kevin Coombs (VATICAN - Tags: RELIGION)
Muumini akipiga mayowe baada ya kutajwa Papa mpyaPicha: Reuters

Maelfu ya waumini tangu Jumanne wamekuwa wakikita kambi katika uwanja wa mtakatifu Petro wakisubiri kuuona moshi mweupe ukifuka kutoka paa la kanisa la Sisitine ambako Makadinali 115 walikuwa wamefungiwa hadi wampate papa mpya na baada ya kupiga kura mara tano,jana usiku saa moja,moshi mweupe ulionekana na kengele katika uwanja huo kupigwa  huku waumini hao wakishangilia kwa vifijo na nderemo.

Wengi walitumai kuwa kwa mara ya kwanza papa mtakatifu atatokea katika eneo tofauti mbali na bara Ulaya huku kadinali kutoka Brazil Odilo Sherer na kadinali kutoka Ufilipino wakipigiwa upatu.

Mjini Buenos Aires kulijaa shangwe punde tu baada ya Papa Francisco wa kwanza kutangazwa kuwa papa mpya.Wengi walitumai kuwa kwa mara ya kwanza papa mtakatifu atatokea katika eneo tofauti mbali na bara Ulaya huku kadinali kutoka Brazil Odilo Sherer na kadinali kutoka Ufilipino wakipigiwa upato. 

Papa Francisco wa kwanza anaelezwa kuwa atakabiliwa na kibarua kigumu cha kurejesha hadhi ya kanisa hilo ambayo imezongwa na kashfa za dhuluma za kingono,ufisadi na malumbano ya wenyewe kwa wenyewe.

Mwandishi:Caro Robi/Afp/Dpa
Mhariri: Sudi Mnette