Papa Benedikt
16 Aprili 2008
Kiongozi wa kanisa katoliki baba mtakatifu, Benedikt wa 16 amesema amefedheheshwa sana na matendo ya makasisi wa kanisa katoliki wa nchini Marekani ya kuwafanya vibaya watoto .
Baba mtakatifu ameeleza hayo kabla ya kuanza ziara yake ya kwanza nchini Marekani kama kiongozi wa kanisa katoliki
Amesema anaazimia kuwazuia waharibifu wa watoto kuwa makasisi. Papa Benedikt wa 16 ameeleza kuwa waharibifu hao watatengwa kabisa na kanisa.
Katika ziara yake nchini Marekani baba mtakatifu Benedikt wa 16 atahutubia Umoja wa Mataifa , ataendesha sala mbili, pia atasali kwenye sehemu iliyoshambuliwa na magaidi tarehe 11 mwezi septemba na atatembelea sinagogi.
Wakati huo huo leo papa Benedikt wa 16 anatimiza umri wa miaka 81.