1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa alaani shambulio la Misri

Kabogo Grace Patricia2 Januari 2011

Shambulio hilo la bomu dhidi ya Kanisa limetokea katika mji wa Alexandria, Misri na kuwaua watu 21.

https://p.dw.com/p/zsTI
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedikto XVI.Picha: AP

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedikto wa Kumi na Sita, jana ameungana na viongozi wengine duniani kulaani shambulio la bomu lililotokea katika Kanisa moja nchini Misri na kuwaua watu 21.

Shambulio hilo ni hujuma za hivi karibuni kufanywa dhidi ya Wakristo katika eneo la Mashariki ya Kati na barani Afrika.

Katika mahubiri yake ya mwaka mpya, Baba Mtakatifu ametoa wito wa kuwepo kwa uhuru wa kuabudu na kuvumiliana, akiwasihi Wakristo kutokataa tamaa katika imani yao kutokana na vitendo vya kibaguzi.

Viongozi kutoka duniani kote, akiwemo Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton na Rais Barack Obama wa Marekani, wamelielezea shambulio hilo kama la kikatili na kutia hofu.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (AFPE,DPAE,RTRE)

Mhariri: Sekione Kitojo